SERIKALI KUENDELEA KUKUSANYA MAONI KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI ILI KUBORESHA KANUNI ZA CSR


                   Na, Mwandishi wetu.

Serikali kupitia Wizara ya Madini imesema ilitunga Kanuni za Wajibu wa Wamiliki la Leseni kwa Jamii (CSR) na kuanza kutumika Mwezi Juni, 2023 zikiwa na lengo la kusimamia utekelezaji wa CSR ambapo kanuni ya 15 (1) imeeleza Mmiliki wa leseni ya madini atawajibika kutekeleza mpango wa wajibu wake kwa jamii kwa kuzingatia taratibu za ununuzi na anaweza kumwajiri mkandarasi au mtu mwingine yeyote katika utekelezaji wa miradi iliyopo.

Majibu hayo ya serikali yametolewa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa leo Januari 27, 2026 wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mheshimiwa Mwita Waitara alilouliza kuwa "Je, lini Kanuni za CSR kwenye migodi zitabadilika ili Miradi ya Maendeleo isimamiwe na Halmashauri kwa mtindo wa Local Fund badala ya Mwekezaji."  

 

"Wizara ya Madini ilitunga Kanuni za Wajibu wa Wamiliki la Leseni kwa Jamii (CSR) na kuanza kutumika Mwezi Juni, 2023 zikiwa na lengo la kusimamia utekelezaji wa CSR ili kuhakikisha Jamii zinazozunguka migodi zinanufaika ipasavyo na uwepo wa migodi husika. Kanuni hizo zimeeleza bayana wajibu pamoja na majukumu ya wadau muhimu wanaohusika na CSR ambao ni Mmiliki wa Leseni (Mgodi) na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Halmashauri).

 

"Katika kutekeleza miradi ya CSR Kanuni ya 15 (1) imeeleza Mmiliki wa leseni ya madini atawajibika kutekeleza mpango wa wajibu wake kwa jamii kwa kuzingatia taratibu za ununuzi na anaweza kumwajiri mkandarasi au mtu mwingine yeyote katika utekelezaji wa miradi iliyopo kwenye mpango. Aidha, Wizara ya Madini imeendelea kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kwa lengo la kuboresha Kanuni za CSR zilizopo." Alisema Naibu Waziri 

 

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA