Na WAF, Dodoma
Waziri
wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa ameiasa jamii kuachana na dhana potofu
ya kuficha wagonjwa wa Ukoma na kujitokeza wanapobaini viashiria vya
ugonjwa huo ili kurahisisha jitihada za Serikali kutokomeza ugonjwa huo
nchini.
Waziri
Mchengerwa amesema hayo leo Januari 25 2025, wakati alipozungumza na
waandishi wa habari akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Ukoma duniani
kwenye ofisi za Wizara Jijini Dodoma.
Waziri
Mchengerwa amewataka Waganga Wakuu wa Miko ana Wilaya kuhakikisha kaya
zote zilizo katika maeneo wanakoibuliwa wagonjwa wapya wa Ukoma
zinafuatiliwa na wanakaya wote kufanyiwa uchunguzi na kubaini wenye
kuugua Ugonjwa huo na kuwaanzishia matibabu.
“Nichukue
fursa hii kuwataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kaya zote zilizo
katika maeneo wanakoibuliwa Wagonjwa wapya wa Ukoma zinafuatiliwa na
wanakaya wote kufanyiwa uchunguzi na kubaini wote wenye kuugua Ugonjwa
wa Ukoma na kuwaanzishia matibabu. Tukifanya hivyo kila Mkoa na
Halmashauri na kila mahali tunaweza kutokomeza ugonjwa huu hata kabla ya
Mwaka 2030,” amesema Mhe. Mchengerwa.
Waziri
Mchengerwa ameitaka Mikoa na Halmashauri kuhakikisha wagonjwa wote
wanaoibuliwa wanatambuliwa makazi, Kijjji, na Kata anakotoka, ndani ya
Wilaya husika au nje ya Mkoa huku akisema iwapo mgonjwa atatokea nje ya
Mkoa, ihakikishwe ya kuwa taarifa zake zinapelekwa alikotokea ili
kufanya ufuatiliaji na kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa Ukoma na
kuwapatia tibakinga kaya husika.
Aidha,
Mhe. Mchengerwa amesema tangu mwaka 2006, Shirika la Afya Duniani (WHO)
limeitangaza Tanzania kuwa tayari imefikia kiwango cha kimataifa cha
kutokomeza ugonjwa wa Ukoma cha chini ya mgonjwa mmoja kati ya watu
10,000 ambapo idadi ya wagonjwa wapya wanaogunduliwa nchini inaendelea
kupungua kutoka wagonjwa 2,297 mwaka 2015 hadi wagonjwa 1442 mwaka 2025
sawa na punguzo la asilimia 37.
Waziri
Mchengerwa amewashukuru watoa huduma katika vituo vya huduma za afya
nchini kwa juhudi za kuboresha afya za wananchi na kuhakikisha ugonjwa
wa Ukoma unapungua kasi ya kusambaa nchini. Huku akiwapongeza wanahabari
kwa kuendelea kuelimisha jamii kuhusu afya bora na namna ya kukabiliana
na magonjwa mbalimbali ukiwemo Ugonjwa wa Ukoma.
“Mikoa
na halmashauri inabidi mhakikishe kila mgonjwa anayeibuliwa
anatambulika anakotoka na taarifa zake zifanyiwe kazi ili kukata
mnyororo wa maambukizi, niwashukuru watoa huduma kwa juhudi zenu za
kutibia wananchi na wanahabari ambao mnasambaza elimu kwa wananchi juu
ya ugonjwa huu,” amesema Mhe. Mchengerwa






Post a Comment