MALENGO YA SERIKALI NI KUZALISHA MEGAWATI 8,000 ZA UMEME IFIKAPO 2030- RAIS SAMIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa hadi kufikia mwaka 2030 Taifa linafikia uzalishaji wa umeme wa megawati 8,000.


Amebainisha hayo leo Februari 09, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uapisho wa viongozi wateule aliowateua tarehe 6 Februari 2026,  akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dkt. James Mataragio.


Ameeleza kuwa kiasi hicho cha umeme kitazalishwa kwa kutumia vyanzo mbalimbali  ikiwemo Jua, Maji na Jotoardhi hivyo amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia umeme na nishati jadidifu kusimamia lengo hilo la Serikali.


Aidha, amemuagiza Dkt. Mataragio kusimamia kwa ukaribu  masuala yote ya gesi na mafuta


Katika hafla hiyo, amewataka viongozi walioapishwa  kufanya kazi kwa kuzingatia viapo walivyoapa huku akiwasisitiza kuimarisha uwajibikaji na kuhakikisha huduma zinaendana na mahitaji na matarajio ya wananchi.






Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA