MANUMBU AANDIKA HISTORIA, AORODHESHWA MIONGONI MWA TOP 100 AFRICANS GLOBAL 2026

 


Kiongozi kijana katika masuala ya Elimu, Habari na Siasa, Dotto Emanuel Manumbu, ametangazwa rasmi kuwa mmoja wa washindi wa tuzo za Top 100 Africans Global 2026, akitambuliwa katika kipengele cha Global Young Male Political Leader.

Tuzo hiyo imetolewa kwa kutambua mchango wake mkubwa katika uongozi na juhudi zake za kuleta maendeleo chanya kwa jamii pamoja na Taifa kwa ujumla. 

Kupitia nafasi mbalimbali za kiuongozi, Manumbu ameonyesha uwezo, ubunifu na dhamira ya dhati katika kutumikia nafasi yake na jamii kwa ujumla. 

Akizungumzia ushindi huo, Manumbu ameeleza kuwa ni heshima kubwa kwake na kwa Tanzania kwa ujumla, akisisitiza kuwa tuzo hiyo ni motisha ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii, unyenyekevu, na uadilifu kwa manufaa ya jamii.

"Tuzo hii ya heshima ni mali ya Mungu anayegawa ridhiki kwetu, nawashukuru sana wazazi, viongozi wangu walio nilea katika utumishi wangu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ukerewe, DC Ngubiagai, DED, Chuo Kikuu bora Afrika cha Mt. Augustine SAUT Tawi la Mwanza kisima cha kuzalisha viongozi makini, pamoja na Watumishi wenzangu wote katika halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kwa malezi mpaka kufikia hatua hii",ameeleza Manumbu.

Hafla rasmi ya ugawaji wa tuzo hizo inatarajiwa kufanyika tarehe 28 Februari 2026 katika ukumbi wa Morena Hotel jijini Dodoma, ambapo washindi kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika watatunukiwa tuzo hizo rasmi.

Ushindi huo umeendelea kuiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa kwa kuonyesha mchango wa vijana katika uongozi na maendeleo ya Bara la Afrika.






Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA