VINARA 16 WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA WATUNUKIWA TUZO



Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF Tanzania), kwa kushirikiana na mtandao wa kupambana na ukatili wa kijinsia (Mkuki) na wadau wengine wa maendeleo, wameandaa na kugawa tuzo kwa vinara 16 wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na utetezi wa haki za binadamu.

Ugawaji wa tuzo hizo umefanyika Februari 05, 2026 jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wawakilishi wa serikali, mabalozi mbalimbali, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wanaharakati wa haki za wanawake, wanasheria, vyombo vya habari na asasi za kiraia,

Akizungumza katika Hafla hiyo, Mkurugenzi wa WiLDAF Tanzania, Wakili Anna Kulaya, alisisitiza kuwa juhudi za kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ni jukumu letu sote ikiwa ni Pamoja na kuwasaidia wote waliopitia ukatili huo. Huku akipongeza hatua ya jamii kubwa ambayo kwasasa haikalii kimya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
“Tumeona viongozi wa jamii wanabadili fikra na kuwa sehemu ya jitihada zetu za kuukata ukatili wa kijinsia hasa baadhi ya mila potofu. Tumeona kuongezeka kwa uelewa wa haki za kisheria na haki za binadamu kiujumla. Kwasasa wanajamii wengi wanavunja ukimya dhidi ya vitendo hivi, wanachukua hatua kudai haki na uwajibikaji”,amesema

Aidha, amepongeza juhudi za serikali katika kuunga mkono mapambano hayo ya uimarishwaji wa mifumo ya utoaji haki ikiwa ni Pamoja na kuongeza idadi ya madawati ya kijinsia, Pamoja na kuongezeka kwa weledi wa kuwahudumia waathirika na wahanga wa vitendo vya ukatili huo.

“Tumeona uimarishwaji wa mifumo ya utoaji haki ikiwa ni Pamoja na kuongeza idadi ya madawati ya kijinsia, Pamoja na kuongezeka kwa weledi wa kuwahudumia waathirika na wahanga wa vitendo vya ukatili huo”, ameongeza Kulaya.

Bi. Kulaya ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau wa maendeleo waliounga mkono kufanikisha zoezi la ugawaji tuzo hizo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha haki za wanawake na watoto, wadau hao ni Ubalozi wa Uswisi, Ubalozi wa Finland, ubalozi wa Ireland, UNFPA, UNICEF, LSF,BRAC, ITV, Coca-Cola Kwanza Ltd, na TBL.




Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA