KIHONGOSI AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA SUKUMA MAGU


Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa (CCM) Taifa, amefanya ziara Mkoani Mwanza na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Sukuma lililopo Kata ya Vaya Wilayani Magu ambalo hadi sasa limefikia asilimia 80 ya utekelezaji.


Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Kihongosi alisema daraja hilo linalojengwa na Serikali I kwa gharama ya Baada you zaidi ya Shilingi bilioni 9 lilikuwa sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.


Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Meneja wa (TANROADS) Mkoa wa Mwanza Ambros Pascal alisema daraja hilo lenye urefu wa mita 70 limefikia asilimia 80 ya ujenzi.


Alieleza kuwa kazi zilizokamilika ni pamoja na ujenzi wa nguzo za katikati (piers), kuta za mwanzo (abutments), nguzo mlalo, ujenzi wa deck slab pamoja na uwekaji wa tabaka la changarawe.


Kihongosi ameanza ziara yake mkoani Mwanza ambapo leo Machi 10, 2026 alipokelewa na mamia ya wananchi katika Kijiji cha Sukuma Wilayani Magu.


Katika mkutano huo aliwafikishia wananchi salamu kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan na kusema alimwambia akifika Mwanza awashukuru wananchi wa mkoa huo kwa kumpa kura za heshima katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA