KIHONGOSI ATAKA VIJANA SENGEREMA KUPEWA ELIMU KUHUSU MIKOPO YA ASILIMIA 10

 

Sengerema, Mwanza.


Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Ndg. Kenan Kihongosi amemtaka Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza Ndg.Alto Mbikiye kutoa elimu kwa vijana kuhusu namna ya kunufaika na mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na halmashauri.


Kihongosi amesema elimu hiyo itasaidia vijana wengi kuelewa utaratibu wa kupata mkopo huo ili waweze kunufaika na asilimia 4 ya fedha hizo iliyotengwa mahsusi kwa ajili ya vijana kwa lengo la kuwawezesha kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi.


Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa, Shina namba 20 katika eneo la Mwabaluhi mkoani Mwanza.


Aidha, amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Ndg.Senyi Ngaga kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa utoaji wa mikopo hiyo ili kuhakikisha vijana wengi wanapata fursa ya kunufaika na mkopo huo.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA