MNEC AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MIRADI YA TACTIC BUKOBA MJINI


Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Kamati kuu ya CCM Taifa kutoka mkoa wa Kagera Ndg. Karim Amri amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za Miradi ya TACTIC inayoyekelezwa Manispaa ya Bukoba.

Karimu  amemtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wa SOKO ili Mradi huo uanze kutoa huduma kwa wananchi wa Bukoba.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo msimamizi wa mradi Nixon Kissa amesemamradi wa ujenzi wa soko kuu Bukoba mjini umefikia asilimia 15%   na kusema watahakikisha wanamaliza kwa wakati.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mhandis Johnston Mutasingwa amemsisitiza mkandarasi kuongeza kasi zaidi ikiwezekana kufanya kazi usiku na mchana ili kuweza kukimbizana na mvua.

Mradi wa Soko kuu Bukoba ni moja ya miradi mitano inayofadhiliwa na Benki Ya Dunia kupitia TACTIC.








Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA