MWILI WA LUKUVI WAFIKISHWA KIJIJINI KWAO IDODI KWAAJILI YA KUMPUMZISHA KESHO MACHI 31, 2026

 

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na Mbunge wa Jimbo la Isimani, Marehemu Mhe. William Lukuvi, wafikishwa Kijijini kwao Idodi mkoani Iringa. 


Mwili wa Mhe. Lukuvi ulisafirishwa kutokea Iringa mjini mara baada ya kufanyiwa Ibada Maalum na kuagwa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Kanisa Kuu - Kihesa, Jimbo Katoliki Iringa leo Machi 30, 2026.


Mhe. Lukuvi alifariki dunia  tarehe 25 Machi, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa kesho Machi 31, 2026 Kijiji Idodi.


















Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA