TANZIA: BWEGE AFARIKI DUNIA



Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilwa Kusini Seleman Bungara (Bwege) amefariki Dunia mchana huu, akiwa kwenye Hospitali moja ya binafsi huko Kigamboni, Dar es Salaam


Kaka wa marehem Abbas S.A. Bungara amesema marehemu alifikishwa Hospitalini hapo kwaajili ya kufanyika Dialysis kama ilivyokuwa ikifanyika kawaida, na ndipo umauti ulivyomfika,

Aidha kwa sasa mipango ya mazishi inaendelea, na taarifa zaidi zitatolewa hapo baadae ila msiba (kwaajili ya watu kuhani) ni Temeke nyumbani kwa Abbas Bungara,

Enzi za uhai wake marehemu Bwege amewahi kutumikia vyama vya siasa vya CUF, ACT Wazalendo na hivi karibuni alitangaza kujiunga na CHADEMA, ingawa mchakato rasmi wa kukabidhiwa kadi ya chama hicho ulikuwa haujakamilika.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA