EWURA YATANGAZA ONGEZEKO LA BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI, SABABU ZAELEZWA


Bei ya mafuta ya petroli imeibua gumzo na maoni mseto katika mkoa wa dar es salaam ambapo imepanda toka shilingi 2,864 kwa lita mwezi Machi hadi kufikia shilingi 3,820 na baadhi wakiuziwa shilingi 4000 kwa lita mwezi Aprili 2026,


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inaeleza ongezeko hilo la zaidi ya shilingi 900 kwa mujibu wa kunatokana na mabadiliko ya soko la kimataifa, likiwemo ongezeko la bei ya mafuta ghafi na changamoto za usafirishaji, gharama za uagizaji na usafirishaji zimeongezeka, zikichangiwa pia na kupanda kwa gharama za bima ya meli pamoja na ucheleweshaji wa mizigo.

Aidha, hali ya kisiasa na kiusalama duniani, hususan mvutano unaoendelea kati ya mataifa mbalimbali, imechangia kuvuruga upatikanaji na usambazaji wa mafuta katika masoko ya kimataifa.

Hata hivyo mpaka sasa kwa wateja wa rejareja mkoani dar es salaam wamejaza lita moja kwa shilingi 4000 hali inayoibua maswali na gumzo maeneo mbalimbali ikiwemo mikoa ya Tanga na Mtwara, ambako bei mpya zimeanza kutumika rasmi kuanzia leo Aprili Mosi mwaka huu.



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA