NAIBU WAZIRI SALOME MAKAMBA ASHIRIKI UJENZI KANISA LA ANGLICAN SHINYANGA


Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba ameshiriki ibada na kukabidhi mifuko 80 ya Saruji katika kanisa la Mtakatifu Stephano Anglican Shinyanga kama sehemu ya kuunga mkono ujenzi unaoendelea katika kanisa hilo.

Salome Makamba amesisitiza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuwajibika kwa jamii na kukuza umoja wa kitaifa baina ya Serikali, Taasisi za Dini na jamii,huku akiahidi kushiriki kwa kila hatua ili kukamilisha ujenzi wa Kanisa hilo.

Ameeleza kuwa Taasisi za Dini zinalo jukumu la kusimamia jamii kiimani hatua itakayo waleta watu pamoja,kudumisha amani, umoja na mshikamano ndani ya jamii.

Akipokea mchango huo Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Johnson Chinyong'ole ametoa shukrani za dhati kwa Naibu Waziri Makamba huku akiweka wazi shauku yake ya kumalizika kwa jengo hilo ili kuruhusu ushiriki mkubwa zaidi na uhuru katika kuabudu kwa waumini wa Kanisa hilo.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA