Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Jesca Kishoa, amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu kufuatia zuio la mikutano ya hadhara lililotolewa na Serikali, akisema shughuli hizo zitaendelea mara tu zuio litakapomalizika.
Kishoa ameyasema hayo Julai 20, 2026, alipokuwa akiwasalimia wananchi katika eneo la Iguguno, wilayani Mkalama mkoani Singida, baada ya wananchi kuuzuia msafara wake ili kuzungumza naye.
"Sasa hivi kuna zuio la mikutano ya hadhara lililotolewa na Serikali. Niwaombe muendelee kuwa wavumilivu, litakapokwisha tutaendelea kufanya mikutano yetu kama kawaida," amesema Kishoa.
Baada ya kuzungumza na wananchi, mbunge huyo aliendelea na ziara yake kwa kutembelea wananchi wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi katika eneo la Iguguno na kusikiliza changamoto zao.









إرسال تعليق