Hatua za kutatua changamoto ya maji katika Kata ya Msingi, Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida, zimeanza baada ya wataalamu wa maji kutoka Mkoa wa Singida kufika katika kijiji cha Kiddii na kufanya ukaguzi wa miundombinu ya maji.
Wataalamu hao wamefika eneo hilo kufuatia maagizo ya Waziri wa Maji, Juma Aweso, yaliyotolewa baada ya Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Jesca David Kishoa, kuwasilisha kilio cha wananchi kuhusu changamoto ya maji katika mkutano wa hadhara.
Katika ziara hiyo, wataalamu hao wamefanya ukaguzi wa maeneo mbalimbali yenye miundombinu ya maji, ikiwemo maeneo yanayohitaji kuboreshwa ili kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi wa Kata ya Msingi kwa ufanisi.
Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi kueleza kwa muda mrefu changamoto wanayokutana nayo katika upatikanaji wa maji, hali iliyomsukuma Mbunge Jesca Kishoa kumtafuta Waziri Aweso moja kwa moja kwa njia ya simu wakati wa mkutano wa hadhara.

إرسال تعليق