Na, mwandishi wetu - Dar es Salaam.
Halmashauri Kuu ya CCM imechukua hatua dhidi ya aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kwa kumvua uanachama wa chama hicho kwamba amekiuka katiba, kanuni na maadili ya chama hicho.
Hatua hiyo imefikiwa leo, Agosti 26, 2026, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, ikiwa ni siku moja baada ya Nchimbi kutangaza kuachia nafasi yake ya Makamu wa Rais na kustaafu shughuli za kisiasa.
Katika mabadiliko hayo ya uongozi, jina la Deogratius Ndejembi limepitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM kuwa pendekezo la kumrithi Nchimbi katika nafasi ya Makamu wa Rais.
Uamuzi huo unakuja wakati CCM ikifanya mabadiliko katika safu zake za uongozi, huku hatua inayofuata ikiwa ni kukamilisha taratibu za kumpata atakayeshika nafasi hiyo Serikalini.

Post a Comment