MBUNGE KISHOA ATOA MIFUKO 200 YA SARUJI UJENZI WA KITUO CHA AFYA, AMPIGIA SIMU WAZIRI AWESO KERO YA MAJI


Na, Mwandishi wetu.


Wananchi wa Kata ya Msingi, Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida, wanatarajiwa kupata ufumbuzi wa changamoto ya maji baada ya Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Jesca David Kishoa, kuwasiliana moja kwa moja na Waziri wa Maji, Juma Aweso, wakati wa mkutano wa hadhara jimboni humo.


Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi kumueleza Mbunge huyo adha wanayoipata kutokana na ukosefu wa maji na kuomba hatua za haraka za kutatua changamoto hiyo.


Akizungumza kwa njia ya simu, Waziri Aweso amepokea malalamiko hayo na kuahidi kutuma wataalamu wa maji wilayani Mkalama leo Jumatatu, kwa ajili ya kufuatilia kwa kina changamoto hiyo na kubaini hatua zinazopaswa kuchukuliwa.


Aidha, kupitia mkutano huo, Mbunge Kishoa ametoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Msingi, hatua inayolenga kusaidia wananchi kupata huduma bora za afya katika eneo hilo.

Akieleza namna wananchi wanavyopokea hatua hiyo pamoja na matarajio yao kuhusu huduma ya maji.


Wananchi sasa wanasubiri utekelezaji wa ahadi hiyo, huku wakitarajia ziara ya wataalamu wa maji itakayosaidia kupata suluhisho la changamoto hiyo kwa muda mrefu.









Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA