RAIS SAMIA AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA NSSF


Kizimkazi, Zanzibar.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Tamasha la Kizimkazi, ambapo alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba.


Pamoja na kutembelea banda la Mfuko, Mhe. Rais alitembelea mabanda mengine ya taasisi na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa.


Mhe. Rais amefurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na NSSF hususan katika kuboresha huduma kwa wanachama.


Katika hatua nyingine,  NSSF imeendelea kutekeleza wajibu wake kwa jamii katika maeneo ya elimu, afya, michezo, jamii, mahitaji maalum na wadau wa maendeleo. Katika tamasha la Kizimkazi, Mfuko umewajibika kwa jamii kupitia utoaji wa majiko janja (80L Electric Pressure Cooker) yanayotumia umeme kidogo sana wastani wa ‘units’ 2 kwa saa nzima , ni salama na yanajizima yakiivisha ambayo yametolewa kwa shule za sekondari sambamba na kushiriki, pamoja na wadau wengine wa maendeleo, katika Kongamano la Nishati Safi lililofanyika hapa Kizimkazi.


Utoaji wa majiko janja na ushiriki wa Mfuko kwenye Kongamano la Nishati safi ni hatua zinazoonesha dhamira ya NSSF ya kuunga mkono Ajenda ya Kitaifa ya Nishati Safi ya Kupikia, inayolenga kuongeza matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kuboresha afya, kulinda mazingira na kuchochea maendeleo endelevu.




Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA