RAIS SAMIA ATHIBITISHA KUJIUZULU KWA NCHIMBI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amethibitisha kupokea barua ya Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ya kujiuzulu nafasi hiyo na kuwa ameridhia ombi hilo.

"Taratibu za kikatiba za kumpata Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwingine zitachukuliwa.


Dkt. Nchimbi ametangaza kujiuzulu kuanzia Septemba 4, 2026, huku akieleza kuwa ameamua pia kustaafu siasa na utumishi wa umma.

Katika barua yake, Dkt. Nchimbi amesema uamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c), ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema uamuzi huo unatokana na ahadi aliyompa Rais Samia Agosti 27, 2025, kwamba angemsaidia kwa uwezo wake wote na kwa uaminifu, lakini angeachia nafasi hiyo endapo Rais angeona kuna haja ya kuwa na Makamu mwingine wa Rais.

Dkt. Nchimbi amesema amejiridhisha kuwa Rais Samia anatamani mabadiliko, hivyo ameamua kutimiza ahadi hiyo.

Ameeleza pia kumshukuru Rais Samia, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Watanzania kwa imani na ushirikiano waliompa katika kipindi chake cha utumishi wa umma.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA