USALAMA WA INTANETI WAFIKISHA ZAIDI YA MILIONI 62 WAKATI FAIBA NYUMBANI IKISALIA NA 178,904



Na Mwandishi Wetu - DAR ES SALAAM,

Takwimu za matumizi ya intaneti nchini zinaonesha fursa kubwa ya upanuzi wa huduma ya intaneti ya kasi majumbani, huku usajili wa intaneti ukifikia 62,793,986 kwa robo mwaka iliyoishia Juni 2026.


Akizungumza Agosti 21,2026 jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Faiba Mlangoni Kwako, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, amesema matumizi ya data nchini yamefikia Petabaiti 1,041, lakini usajili wa huduma ya Faiba Nyumbani ulikuwa 178,904.

Amesema takwimu hizo zinaonesha bado kuna nafasi kubwa ya kukuza huduma ya intaneti ya kasi kupitia teknolojia ya nyuzi za macho.

Waziri ameitaka TTCL kutumia fursa hiyo kwa kupanua huduma hadi maeneo yenye makazi yanayokua, maeneo ya biashara, viwanda, shule, vyuo, vituo vya afya na ofisi za Serikali.

Pamoja na upanuzi huo, ameitaka TTCL kuhakikisha huduma inabaki kuwa bora, ya uhakika na yenye gharama nafuu.


Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, CPA Moremi Marwa, amesema Awamu ya Pili inalenga kuongeza zaidi ya Home Pass 400,000, baada ya Awamu ya Kwanza kufikisha zaidi ya 280,000.

Amesema matumizi ya teknolojia ya GPON yatawezesha TTCL kuwahudumia wateja wengi zaidi na kuboresha ufanisi wa matumizi ya miundombinu ya nyuzi za macho.






Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA