WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KIZOTA WAPATIWA CHANJO DHIDI YA POLIO



Na Jesca Kipingu, KIZOTA

Wataalamu wa afya kutoka Kituo cha Afya Kizota wamefika katika Shule ya Msingi Kizota, Kata ya Kizota, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kutoa chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi 0 hadi miaka 10, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa huo na madhara yake.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Katibu wa Afya katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambaye pia ni Msimamizi wa Kampeni ya Chanjo ya Polio, Hapiness Kaungya, aliwashukuru wazazi kwa mwitikio mkubwa na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na wataalamu wa afya.

Kwa upande wake, Afisa Muuguzi Msaidizi II, Naomi Simon, alisema zoezi hilo limekuwa na mwitikio mzuri, huku akiwahimiza wazazi kuhakikisha watoto ambao bado hawajapatiwa chanjo wanapata huduma hiyo kwa wakati.

Naye Kiongozi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) wa Kata ya Kizota, Kabla Pima, aliwapongeza wazazi kwa ushirikiano wao, huku Mwalimu wa Afya wa Shule ya Msingi Kizota, Mwl. Adelmas Mmbando, akihimiza jamii kuondokana na dhana potofu kuhusu chanjo.

Kwa ujumla, zoezi hilo limeonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya wataalamu wa afya, shule, wazazi na jamii katika kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kuanzia miezi 0 hadi miaka 10 anapatiwa chanjo dhidi ya Polio kwa ajili ya kulinda afya na ustawi wake.





Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA