BOCHELA WAPEWA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Na. Mwandishi Wetu, DODOMA


Wananchi wa Mtaa wa Bochela, Kata ya Nkuhungu, Jijini Dodoma, walipatiwa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia, aina zake, madhara pamoja na umuhimu wa kutoa taarifa kuhusu vitendo hivyo katik siku ya afya na lishe ya mtaa(SALiKI).


Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo, Inspekta Amina Shabani Polisi Kata ya Nkuhungu, alieleza kuwa ukatili wa kijinsia unahusisha  matendo mbalimbali yanayosababisha  mtu mateso au madhara kwa njia ya kimwili, kingono, kiuchumi au kihisia.


Alifafanua kuwa miongoni mwa aina za ukatili wa kijinsia zilizotolewa elimu zilikuwa ukatili wa kimwili, ukatili wa kingono ikiwemo kulawitiwa, ukatili wa kiuchumi pamoja na ukatili wa kihisia.


Inspekta Amina Shabani aliwahimiza wananchi kuwa na uelewa kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutokaa kimya wanapobaini  matukio hayo, badala yake wanatakiwa  kutoa taarifa kwa vyombo husika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.


Aidha, alisisitiza umuhimu wa jamii kushirikiana katika kuzuia vitendo vya ukatili na kulinda watoto, wanawake pamoja na makundi mengine yaliyokuwa katika mazingira hatarishi.


Elimu hiyo ilitolewa ikiwa ni sehemu ya shughuli za uhamasishaji kwa wananchi wa Mtaa wa Buchela, kwa lengo la kuongeza uelewa wa jamii kuhusu namna ya kutambua, kuzuia na kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia.






Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA