HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA YAFANYA MAREKEBISHO YA BARABARA YA KUINGIA STENDI YA MNADANI KIZOTA



Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea na zoezi la kufanya marekebisho ya barabara ya kuingia katika Stendi ya Mnadani Kizota, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule.


Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuzungumza na wamiliki wa daladala na bajaji jana, ambapo alisisitiza umuhimu wa vyombo hivyo kuingia na kupaki ndani ya stendi badala ya kusimama na kupaki nje ya eneo la stendi, hali ambayo ni kinyume na utaratibu na sheria zilizowekwa.


Halmashauri imeanza kuchukua hatua za haraka kuhakikisha mazingira ya kuingia na kutoka katika Stendi ya Mnadani Kizota yanakuwa rafiki na salama kwa daladala, bajaji, abiria na watumiaji wengine wa barabara.


Marekebisho hayo yanatarajiwa kurahisisha utekelezaji wa maelekezo hayo na kuhakikisha Stendi ya Mnadani Kizota inatumika kwa utaratibu unaostahili, huku ikisaidia kupunguza msongamano na usumbufu unaoweza kujitokeza nje ya stendi.


Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea kusisitiza kwa wamiliki na waendesha vyombo vya usafiri kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya mamlaka husika katika kuhakikisha usafiri wa umma unafanyika kwa usalama na utaratibu.






Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA