Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Jesca David Kishoa, amefanya ziara katika Kata ya Nkinto, Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi wa eneo hilo.
Katika mkutano huo, wananchi wamewasilisha changamoto mbalimbali, ikiwemo huduma za afya pamoja na miundombinu ya barabara, huku Kishoa akimtaka afisa mipango ambae alikuwa mwakilishi wa afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri kutoa majibu kuhusu changamoto za afya zilizowasilishwa na wananchi.
Aidha, ameitaka TARURA Wilaya kutoa majibu ya kina kuhusu hali ya barabara na maandalizi yake kuelekea msimu wa mvua za El Niño, ili kuhakikisha wananchi wanapata usafiri bila changamoto kubwa.
Miongoni mwa wananchi walioeleza changamoto zao ni Julias Gerson, ambaye amesema amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kutokwa na mkojo kwa kipindi kirefu na kumuomba msaada mbunge huyo ili aweze kupata matibabu.
Akijibu ombi hilo, Kishoa amesema yuko tayari kumsaidia Julias kwa kumfikisha katika kituo cha matibabu ili aweze kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu yanayohitajika.
.jpeg)
Post a Comment