Na, Mwandishi wetu.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limeanza uchunguzi kuhusu picha inayosambaa mitandaoni ikimuonyesha kijana Giles George Handi, mkazi wa Nkasi, akiwa amefungwa pingu.
Taarifa ya Jeshi hilo ya Septemba 23, 2026, imeeleza kuwa picha hiyo imeambatana na madai kwamba kijana huyo amekuwa na pingu hizo kwa muda wa siku tatu.
Polisi imesema uchunguzi unafanyika ili kubaini ukweli wa tukio hilo na mazingira yaliyosababisha kufungwa kwake.
Aidha, Jeshi hilo limewataka wananchi kuwa na subira wakati uchunguzi ukiendelea na kuahidi kuchukua hatua stahiki endapo itabainika kuwa kuna ukiukwaji wa sheria au taratibu.
إرسال تعليق