RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MUDA HUU

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi katika nafasi mbalimbali za Serikali.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo umehusisha nafasi za uwaziri, uongozi wa Serikali na taasisi mbalimbali.


Mhe. Masanja Kungu Kadogosa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi, akichukua nafasi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mhe. Abdallah Hamis Ulega.


Mhe. Ulega ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Waziri wa Ujenzi.


Aidha, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera ameteuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Homera alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.


Katika uteuzi huo, Bi. Asha Khamis Abdulla ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia masuala ya usimamizi wa fedha.



 


Prof. Bruno Fokas Sunguya ameteuliwa kuwa Mganga Mkuu wa Serikali, huku Bw. Jabiri Omari Makame akiteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).


Vilevile, Dkt. Idrissa Muslim Hija ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA