SERIKALI KUONDOA SHERIA KAKASI KATIKA UWEKEZAJI WA MALI ASILIA NA MALIASILI

 

Serikali, kupitia Wizara ya Katiba na Sheria, imeweka mkakati wa kuondoa sheria kakasi zinazorudisha nyuma masuala ya uwekezaji katika mali asilia na maliasili za nchi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.


Hayo yamebainishwa Septemba 7, 2026, na Mkurugenzi wa Kitengo cha Usimamizi wa Mali Asilia na Maliasili za Taifa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Neema Mwanga, wakati akihojiwa na waandishi wa habari kwenye Kongamano la 5 la Kimataifa la Kisayansi la Uchumi wa Buluu linalofanyika jijini Dar es Salaam.


Wizara ya Katiba na Sheria inashiriki katika kongamano hilo la siku tatu, linalofanyika kuanzia Septemba 7 hadi 9, 2026, ikiwa ni mdau muhimu katika kutoa elimu kuhusu namna Serikali inavyoendelea kuhakikisha sheria, kama nyenzo kuu ya uwekezaji, zinakuwa rafiki na wezeshi katika kuchochea uwekezaji na kufikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya 2050.



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA