DKT. MWIGULU ATEMBELEA VYLOR, AJADILI MASUALA YA UZALISHAJI WA MBEGU BORA



Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, jana Oktoba 23, 2026, ametembelea kampuni ya Vylor inayojihusisha na utengenezaji wa mbegu za kisasa za kilimo, ambayo zamani ilikua sehemu ya Corteva Agriscience mjini Johnston, Jimbo la Iowa, nchini Marekani.

Akiwa katika kampuni hiyo ambayo pia imejikita katika uwekezaji wa teknolojia ya vinasaba na utafiti wa kilimo, Dkt. Mwigulu amefanya mazungumzo ya pamoja na wawakilishi wa kampuni hiyo kuhusu shughuli wanazozifanya katika bara la Afrika ikiwa ni pamoja na Tanzania.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu amepokea maelezo kuhusu utaalamu, utafiti na teknolojia za kampuni hizo zinazohusisha uzalishaji wa mbegu bora sambamba na teknolojia ya kuzuia wadudu wanaoshambulia mazao ya kilimo.

Wawakilishi wa Vylor pamoja na mambo mengine walieleza kwamba Tanzania ni moja kati ya nchi sita za Afrika ambazo wanapanga kuongeza wigo wa shughuli zao.


Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe; na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA