Na Mwandishi Wetu – Dodoma
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Uratibu na Wenye Ulemavu kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS),
imeendelea kuongeza kasi ya upimaji wa Virusi vya Ukimwi (VVU) na kujikinga
dhidi ya virusi hivyo kwa kuongeza kasi ya afua za kinga, upimaji na matibabu,
ikiwa ni sehemu ya jitihada za kutokomeza UKIMWI kama tishio la afya ya umma
ifikapo mwaka 2030.
Hatua hizo zimeelezwa Oktoba 22, 2026
Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Uratibu na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, wakati akiwasilisha taarifa
ya utekelezaji wa afua za kudhibiti maambukizi ya VVU na UKIMWI katika mikoa
yenye kiwango cha juu na chini cha maambukizi,
na taaarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza la Taifa la Watu
Wanaoishi na VVU Tanzania (NACOPHA) katika kipindi cha Januari 2021 hadi
Septemba 2026, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI.
Waziri Kabudi ameeleza kuwa katika
jitihada za kuhakikisha kwamba nchi inafikia malengo ya kuuondoa UKIMWI kama
tishio la afya kwa umma ifikapo mwaka 2030, Tanznaia imeweza kuendeleza afua
mbalimbali katika mwitikio wa kupambana na VVU na UKIMWI, ikiwemo kufufua
kiwanda cha kutengeneza dawa na vifaa tiba cha Tanzania Pharmaceutical
industries Ltd (TPI) kilichopo mkoani Arusha, ambacho kinazalisha dawa za
kufubaza makali ya VVU (ARV) na hivyo kuleta uhakika wa upatikanaji wa huduma kufubaza
VVU.
Kwa upande mwingine, Mheshimiwa Waziri amesisitiza
ushirikiano kati ya Serikali, TACAIDS, NACOPHA, Serikali za Mitaa, asasi za
kiraia, sekta binafsi, washirika wa maendeleo na jamii, katika kuongeza uelewa,
kupunguza unyanyapaa na kuhakikisha huduma za kinga na matibabu zinawafikia
vijana, wanawake na makundi yaliyo katika mazingira hatarishi ya kuoata
aambukizi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa
TACAIDS, Dkt. Adam Mrisho amesema Tanzania imepiga hatua katika kupunguza
maambukizi mapya ya VVU, vifo vitokanavyo na UKIMWI, maambukizi kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto na kuimarisha upatikanaji wa huduma za kinga, tiba na matunzo.
“Lengo ni kuhakikisha vifo venabaki kua
vichache. Waliokua na VVU wamefubaza VVU kwa kuhakikisha wametumia dawa vizuri
na wasiweze kuambukiza wengine” amesema Dkt. Mrisho.
Naye, Mtendaji Mkuu wa NACOPHA Bw.
Deogratius Rutatwa ameishukuru serikali kwa upatikanaji wa huduma za matibabu
na dawa kinga, hali inayofanya watu wanaoishi na VVU waishi kwa kujiamini na
sio kwa matumaini.
Serikali inaendelea kutekeleza afua
mbalimbali ikiwemo upimaji wa VVU, usambazaji wa kinga, tohara salama na hiari
kwa wanaume, kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,unyanyapaa, na
huduma za matibabu na Matunzo.



.jpeg)
.jpeg)
إرسال تعليق