WAZIRI MKUU KUFUNGUA JUKWAA LA UWEKEZAJI TANZANIA NCHINI UINGEREZA.


Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameondoka nchini leo, Oktoba 6, 2026, kuelekea Uingereza kwa ziara ya kikazi ya siku tano, ambapo atafungua Jukwaa la Uwekezaji la Tanzania nchini Uingereza. 


Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu pia ataongoza ujumbe wa Tanzania kukutana wadau, wawekezaji na viongozi wa kampuni mbalimbali katika sekta za madini, benki, Teknolojia, usafirishaji na miundombinu, kwa lengo la kuimarisha na kutangaza fursa za Biashara na Uwekezaji.


Jukwaa hilo litatoa fursa kwa Tanzania kutangaza vipaunbele vya Dira 2050 katika nyanja za uwekezaji na kueleza hatua zinazochukuliwa na serikali kuboresha mazingira ya biashara. Ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na kuwakaribisha, Wadau, Wawekezaji na wafanya biashara kushiriki katika miradi mbalimbali nchini.


Jukwaa hilo limelenga kuvutia mitaji na teknolojia, kukuza ujuzi na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania, pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya miundombinu ikiwa ni utekelezaji wa Dira 2050


Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha diplomasia ya uchumi, kuvutia uwekezaji na kusimamia Sera ya maendeleo kwa manufaa ya Watanzania.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA