WADAU WA TIBA ASILIA WAUNGANA KUTAFUTA SULUHISHO LA KISAYANSI

 


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewakutanisha wadau wa tiba asilia, watafiti, wanasayansi, wataalamu wa afya, taasisi za utafiti na wawekezaji katika kongamano la kujadili namna sayansi na utafiti utakavyotumika kuimarisha tiba asili.

Kongamano hilo linatarajiwa kuja na mapendekezo yatakayokuwa msingi wa kuandaa mfumo wa kitaifa wa kubaini, kutafiti kuendeleza ugunduzi na ubiasharishaji wa dawa na vifaa tiba vinavyobuniwa nchini.


Akizungumza Novemba 09, 2026 jijini Dar es salaam wakati wa kufungua kongamano hilo Naibu Waziri wa Elimu, 
Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, aliyemwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Adolf Mkenda, amesema kongamano hilo ni pia ni jukwaa muhimu la kuunganisha wadau na kuweka mikakati ya kutumia sayansi, teknolojia na ubunifu katika masuala ya tiba asili ili ziwe na zimetafitiwa kisayansi

Amesema Tanzania imejaliwa kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali za asili, hususan mimea yenye viambato vinavyoweza kutumika kutengeneza dawa, sambamba na uwepo wa wataalamu wa tiba asilia wenye maarifa na uzoefu mkubwa, lakini bado haijatumia ipasavyo fursa zilizopo katika utafiti, uendelezaji na uzalishaji wa dawa zinazotokana na rasilimali hizo.

Ameeleza kuwa hali hiyo inachangiwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kutokukusanywa na kuhifadhiwa kwa maarifa ya tiba asilia, kutofanyika kwa tafiti za kutosha kuthibitisha usalama na ufanisi wa tiba hizo, pamoja na udhaifu wa ushirikiano kati ya watafiti, vyuo vikuu, mamlaka za udhibiti na viwanda katika kuendeleza matokeo ya tafiti hadi kuwa bidhaa.

Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha matokeo ya tafiti za tiba asili zinazofanyika katika vyuo vikuu na taasisi za utafiti hayaishii katika machapisho ya kitaaluma na mijadala ya kisayansi, bali yanageuzwa kuwa bunifu, bidhaa na teknolojia zitakazoboresha huduma za afya, kuongeza ajira, kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ili pia kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Kongamano la kuendeleza Sayansi katika nyanja ya tiba asili lina kauli Mbiu Kutumia ubunifu, utafiti na maarifa asilia ya ndani kwa ajili ya maendeleo ya tiba na bidhaa za afya.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA