Waziri wa Nishati, Dkt. Juma Homera, ametangaza kuwa huduma ya umeme katika mikoa ya Mbeya na Songwe imerejea tangu saa kumi usiku, baada ya kukatika kutokana na hitilafu katika njia ya kusafirisha umeme ya Makambako Mbeya.
Kwa mujibu wa taarifa ya awali, hitilafu hiyo ilitokea Novemba 21, 2026, baada ya mnara wa njia ya umeme ya kilovolti 400 uliokuwa ukijengwa kuangukia na kuharibu mnara wa njia ya kilovolti 220 inayosambaza umeme katika mikoa hiyo miwili.
Kufuatia tukio hilo, TANESCO ilituma wataalamu na vifaa kutoka Dar es Salaam kwenda eneo la tukio kwa ajili ya kujenga mnara wa muda ili kurejesha huduma. Akitangaza kurejea kwa umeme, Dkt. Homera aliwapongeza wahandisi wa TANESCO na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Lazaro Twange, kwa kazi hiyo.

Post a Comment