TIMU YA KAMBA, NETIBOLI TAMISEMI ZATINGA HATUA YA MTOANO

 

Na. Asila Twaha, Iringa



Timu ya wanawake ya kuvuta kamba na netiboli  TAMISEMI zimeingia hatua ya mtoano baada ya kucheza mechi 4  na kushinda kupata nafasi nzuri  kwa timu zote mbili  kuingia hatua hiyo.


Mapema asubuhi Oktoba 3, 2023 katika viwanja vya Mkwawa Mkoani Iringa timu ya kamba ilicheza na wapinzani wake Wakili  Mkuu na kuwashinda kwa pointi 2-0 huku timu ya netiboli kucheza katika uwanja wa Chuo Kikuu cha RUAHA kuwafunga wapinzani wao Ujenzi  goli  29-21. 


Kocha wa timu ya kamba TAMISEMI Chediel Masinga amesema pointi 7 walizoshinda kwa mechi nne walizocheza zimewapa nafasi kuingia katika hatua ya mtoano.


Amesema kwa hatua ya makundi  timu ya  TAMISEMI ilipangwa kundi F  kucheza  na RAS Kagera, Mashtaka, Mambo ya Nje na Wakili Mkuu na mechi zote hizo wamefanya vizuri.


Kwa upande wa timu ya netiboli  kushinda na kufikia hatua ya mtoano walicheza na  timu ya  Mashtaka,TARURA,Ujenzi na Uchukuzi.


Michezo ya Shirikisho ya Wizara na Idara za Serikali yatafunguliwa tarehe 4 Oktoba, 2023.

Matukio Katika Picha Wakati wa Mchezo huo ukiendelea.














Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA