Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Masoud Ali Abdala (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima kizungumza.
Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele
Mgombea Mwenza, Mhe. Masoud Ali Abdala
Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele akiwana na Mgombea Mwenza, Mhe. Masoud Ali Abdala (kushoto)
Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele akielekezwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg Ramadhani Kailima namna ya kujaza kitabu.
Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele akisaini kitabu.
Mgombea Mwenza, Mhe. Masoud Ali Abdala akisaini kitabu.
Wajumbe wa Tume pamoja na Menejiment wakiwa katika zoezi la utoaji fomu.
Wanachama wa CCK wakiwa katika utoaji fomu.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza.
David Daud Mwaijojele, amechukua rasmi fomu ya kugombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama Cha Kijamii (CCK)katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, baada ya Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kutangaza dirisha la uchukuaji wa fomu kwa wagombea urais.
Akizungumza mara baada ya kukamilisha taratibu zote katika makao makuu ya NEC jijini Dodoma leo Agosti 12,2025, Mwaijojele amemshukuru Mwenyekiti wa Tume na watendaji wake kwa kuendesha mchakato huo kwa utaratibu mzuri, uwazi na ufanisi.
“Nawashukuru INEC kwa maandalizi bora na usimamizi wa kitaalamu wa zoezi hili,hii ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba,” amesema.
Mwaijojele ameeleza kuwa CCK imejipanga kuendesha kampeni zinazolenga masuala yenye kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja, akitaja vipaumbele vikuu kuwa ni kuendeleza kilimo cha kisasa, kuongeza ajira hasa kwa vijana, kuboresha elimu, pamoja na kuimarisha ustawi wa wastaafu.
Amesisitiza kuwa sera za chama chake zitaweka mazingira rafiki yatakayo wezesha wastaafu kustaafu kwa kujiamini na kuishi kwa amani, akisema wastaafu wengi huingiwa na hofu kutokana na changamoto za kiuchumi baada ya kustaafu.
Katika sekta ya kilimo, Mwajojele amesema CCK itahakikisha upatikanaji wa pembejeo bora, masoko ya uhakika na teknolojia ya kisasa ili kuongeza tija na kipato cha wakulima huku akiahidi elimu walimu na ubora wa mitaala.
Mwajojele atakuwa akiwania nafasi ya urais akiwa na mgombea mwenza, Masoud Ali Abdalla, ambaye ameahidi kushirikiana naye kikamilifu kutekeleza sera na mikakati ya chama.
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu umepangwa kufanyika Oktoba 2025, na zoezi la uchukuaji wa fomu kwa wagombea litaendelea kwa muda uliopangwa na NEC.
إرسال تعليق