MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel
Nchimbi amesema kuwa sekta ya Elimu, hususan elimu ya Juu ina mchango
mkubwa katika uchumi wa Taifa, kutokana na kuzalisha nguvukazi
inayoshiriki kutoa huduma katika sekta mbalimbali.
Mhe.
Nchimbi ametoa kauli hiyo Disemba 15, 2025 Mkoani Kagera baada ya
kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kampasi ya Kagera ya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM), kutokana na mchango huo, Serikali imejizatiti
kuleta mageuzi ya elimu katika ngazi zote, ili kuhakikisha kuwa wahitimu
wanapata ujuzi, stadi na maarifa yanayoendana na soko la ajira.
"Rai
yangu kwa UDSM, hakikisheni Kampasi hii mpya inakuwa kitovu cha
uvumbuzi na ubunifu; kuwawezesha vijana wetu kuibua mawazo mapya,
kufanya ubunifu, na kutumia fursa za soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika
Mashariki’’ Amesema Dkt. Nchimbi.
Mhe.
Nchimbi ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuratibu
mradi mkubwa wa HEET kwa kuhakikisha matumizi adili ya fedha na kwa
kuzingatia thamani ya fedha.
Ameitaka
Wizara kushirikiana na wadau kuandaa mapema mahitaji kama vile
ithibati, vifaa na rasilimaliwatu, ili kuwezesha shughuli za mafunzo
katika Kampasi hiyo kuanza kama ilivyopangwa bila kuchelewa
Pia
ameipongeza UDSM, kwa kusimamia mchakato wa ujenzi wa Kampasi hiyo,
ameitaka kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika matumizi bora ya
rasilimali na utoaji wa elimu yenye tija kwa kizazi cha leo na kesho.
"Hapa
niwatake wasimamizi mkabdarasi na wote wanauhusika kuhakikisha ujenzi
unakamilika kwa wakati uliopangwa hatutavumilia ucheleqaji wowote".
Amesema
Ameishukuru
Benki ya Dunia kwa kushikiriana na Serikali kufadhili utekelezaji wa
mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), ambao umewezesha
ujenzi wa Kampasi ya Kagera hukua akiahidi uwekezaji katika kukamilisha
jengo la abweni la wanafunzi wa kiume na miundombinu mingine muhimu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt.
Jakaya Kikwete amesema kuwepo kwa Chuo hicho kutakuwa kichocheo cha
fursa za kiuchumi na uwekezaji wa Mkoa wa Kagera.
"Nimeambiwa
bei ya viwanja na ardhi katika maeneo yanayozunguka Chuo imepanda
maradufu. Lakini pia kutakuwepo na mahitaji ya Hosteli kwa wanafunzi na
nyumba za kupanga kwa wafanyakazi wa Chuo.
Nawaomba ndugu zangu Wanabukoba mchangamkie fursa hizo". Amesema Dkt. kikwete.
Aidha
ameeleza kuwa Chuo hicho kinaanza kama Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam lakini matumaini yetu ni kuwa siku za usoni kampasi hiyo inaweza
kuja kuwa Chuo Kikuu ambapo akatolea mfano Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) na Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) navyo vilianza kama Kampasi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
lakini leo hii ni Vyuo Vikuu vinavyojitegemea.
"Imekuwa
hivyo kwa MUHAS na SUA kutokana na nia ya dhati ya Serikali kuendelea
kuwekeza na kuwezesha Kampasi hizo kukua na kutanuka. Naamini na sina
shaka kuwa itakuwa hivyo kwa Kampasi hii pia, miaka ijayo". Ameeleza.
Naye
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema
ujenzi wa Kampasi ya Kagera utaongeza fursa za udahili kwa wanafunzi,
kuchochea ukuaji wa uchumi wa eneo husika na kuimarisha matumizi ya
teknolojia pamoja na tafiti katika Kanda ya Ziwa.
Waziri Mkenda amesema kampasi hiyo inatarajiwa kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya elimu na sekta za uzalishaji.
Amesema
Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ni mradi mkubwa wa
kimkakati unaolenga kubadilisha mfumo mzima wa elimu ya juu nchini na
kuufanya kuwa injini ya uchumi wa kisasa.









Post a Comment