Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mara Ndg.Marwa Mathayo akiwa ameambatana na Mhe.Mwita Waitara (Mb)-Tarime Vijijini pamoja na Wabunge wa Viti Maalum Mhe.Ghati Chomete (Mara), Mhe.Dkt.Christina Mnzava (Shinyanga) na Mhe.Suma Fyadomo (Mbeya) Leo tarehe 15 Desemba, 2025 wameshiriki Mazishi ya Marehemu SAMSON WILFRED NYIHITA katika Kitongoji cha Kyabunyonyi, Kijiji cha Nyanchabakenye, Kata ya Kisumwa, Wilayani Rorya, Mkoani Mara.
Viongozi hao wameshiriki Mazishi hayo kwa lengo la kumfariji Ndg.Nyihita Wilfred Nyihita (Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mjumbe wa Baraza la Wazazi Mkoa Mara) ambaye Marehemu ni mdogo wake.
Mazishi hayo yameongozwa na Mkuu wa Wilaya Rorya Mhe.Dkt.Khalfan Haule.

Post a Comment