Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
amewaongoza waombolezaji kwenye Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, yaliyofanyika katika Kijiji cha
Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma leo tarehe 16 Desemba 2025.
Akitoa
salamu za rambirambi mara baada ya mazishi hayo, Makamu wa Rais amesema
marehemu Jenista Mhagama alikuwa mtumishi wa kweli wa watu wake ambaye
aliwatumikia na kuwajali.
Amesema Serikali, Wananchi na Chama cha
Mapinduzi, wamepoteza mtu muhimu ambaye mchango wake hautasauhaulika
katika nyadhifa mbalimbali ambazo amewahi kutumika.
Makamu wa Rais
ameongeza kwamba Serikali na Chama Cha Mapinduzi itaendelea kuenzi
mchango wa marehemu Jenista Mhagana kwa kuendelea kuwa watetezi wa
wananchi wa chini, ambapo ametoa wito kwa Viongozi wa Serikali
kuhakikisha wananchi wa hali ya chini ndio wanakuwa kipaumbele chao cha
kila siku.
Aidha Makamu wa Rais amewasilisha salamu za shukrani
za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
alizozitoa kwa familia na wananchi wa Ruvuma kwa ujumla kutokana na
maisha ya marehemu Jenista Mhagama.
Amesema Rais Dkt. Samia ameguswa sana na msiba huo kutokana na mchango aliotoa marehemu Jenista Mhagama enzi za uhai wake.
إرسال تعليق