
Naibu Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amewasisitiza
maofisa habari nchini kuimarisha uwajibikaji wao kwa kutoa taarifa za
mara kwa mara kwa wananchi kuhusu shughuli zote zinazotekelezwa na
Serikali, katika maeneo yao.
Makonda ametoa kauli hiyo leo
Desemba 15, 2025, jijini Dodoma, alipokutana na Menejimenti ya Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji
wa Serikali Mtumba.
Amesema Wizara ya Habari ni kiungo muhimu
kati ya Serikali na wananchi katika kutangaza, kufafanua na kusemea
utekelezaji wa ahadi na mipango ya maendeleo, hivyo maofisa wake
wanapaswa kutimiza wajibu wao kwa weledi, uwazi na kwa kuzingatia
masilahi ya umma.
“Wananchi wana haki ya kujua kinachofanyika na
Serikali yao. Maofisa Habari mna wajibu wa kuhakikisha taarifa sahihi,
kwa wakati na zilizo wazi zinawafikia wananchi ili kuimarisha uelewa na
imani kwa Serikali,” amesema.
Kwa upande wake, Menejimenti ya
Wizara imeahidi kuendelea kushirikiana na maofisa habari katika ngazi
zote ili kuboresha mifumo ya mawasiliano ya Serikali, ikiwamo matumizi
ya majukwaa ya kidijitali, ili wananchi wapate taarifa kwa haraka na kwa
ufanisi.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603
إرسال تعليق