Na, mwandishi wetu.
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi amesema CCM haitapoteza muda kujibu propaganda zinazoenezwa na watu wasiolitakia mema Taifa, badala yake itaendelea kuzingatia wajibu wake wa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
Akihutubia wananchi wa Iguguno katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Mkalama, leo Januari 20, 2026, Kihongosi amesema msimamo wa Chama ni kuendelea kufanya kazi kwa weledi bila kuyumbishwa na maneno ya kuchochea au ya kupotosha.
"Tumekubaliana ndani ya Chama hatutahangaika kudili na kujibu propaganda za watu wasioitakia mema nchi yetu. Kazi yetu na mkataba wetu ni kwenda kusimamia utekelezaji wa Ilani, maendeleo yaende kwa wananchi. Hamtatusikia tukitukana huko, hamtatusikia tukipayuka huko," amesema.
Amesisitiza kuwa nguvu yote ya CCM itaelekezwa katika kusukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na juhudi za serikali.
إرسال تعليق