Na, Mwandishi wetu - Singida
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amesema Chama hicho hakitasita kuchukua hatua pindi itakapobainika kuna uzembe katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kihongosi ametoa kauli hiyo leo Januari 20, 2026, wakati akizungumza na Mabalozi wa Shina namba 8 katika eneo la Iguguno, wilayani Mkalama, mkoani Singida, ambapo ameweka wazi kuwa wajibu wa kwanza wa CCM ni kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yanayogusa maisha yao moja kwa moja.
Amesema ufuatiliaji wa miradi ya serikali ni jukumu la chama, na kwamba kila fedha inayotolewa lazima ionekane kwenye ubora wa mradi husika.
"Tutaangalia ubora na fedha iliyoletwa, na kama kuna uzembe wa aina yoyote tutachukua hatua mara moja, kwa sababu chama hiki wajibu wake ni kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo," amesema Kihongosi.
إرسال تعليق