Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, ametoa wito kwa wananchi wa Iguguno na Wilaya ya Mkalama kwa ujumla kudumisha umoja, upendo na mshikamano, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda miundombinu ya maendeleo iliyojengwa kwa gharama kubwa.
Akizungumza leo Januari 20, 2026, wakati alipotembelea ujenzi wa Zahanati ya Iguguno wilayani Mkalama, Kihongosi amesema wananchi wametoa nguvu na mchango mkubwa, ikiwemo zaidi ya Sh. milioni 12, hivyo hakuna sababu ya kuruhusu mtu yeyote kuiharibu miundombinu hiyo.
Amesema kitendo cha kuchoma au kuharibu kituo cha afya ni sawa na kuwatakia madhara wananchi, hasa kina mama wanaohitaji huduma za uzazi na wananchi wanaotegemea matibabu ya karibu.
“Unapounguza jengo hili maana yake unawaambia akina mama kwamba nataka mfe, kwa sababu watajifungulia wapi, watatibiwa wapi,” amesema.
Ameongeza kuwa mali za umma ni mali za wananchi na zinatokana na kodi zao, hivyo ulinzi wake ni wajibu wa kila mmoja.

Aidha, Kihongosi amewatahadharisha wananchi dhidi ya kurubuniwa kufanya vurugu au uharibifu wa mali, akibainisha kuwa mara nyingi wachochezi hawatoki Mkalama bali hutoka mbali na kuwaletea chuki zisizo na manufaa.
“Vurugu ya aina yoyote isiwe kipaumbele katika wilaya hii ya Mkalama. Mnahitaji huduma bora, lakini wengi wanaofanya fujo na kuchochea chuki hawaishi hapa Mkalama; wanakuja tu kuwashawishi na ninyi bila kutambua mnafuata mkumbo,” amesema Kihongosi
إرسال تعليق