Waziri
wa Nishati na Maendeleo ya Madini kutoka nchini Uganda Dkt. Ruth
Nankabirwa yuko nchini kwa ziara rasmi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
bomba la kusafirisha mafura ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi
Chongoleani mkoani Tanga, ili kujionea hatua zilizodfikiwa kwa upande wa
utekelezaji nchini Tanzania sambamba na mwenyeji wake Mhe. Deogratius
Ndejembi.
Akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi wa Habari, Waziri wa Nishati Mhe.
Deogratius Ndejembi amesema, kupitia mradi wa EACOP utaleta manufaa
makubwa kwenye ajira, ambapo jumla ya ajira 12,000 zimetolewa kwa vijana
na wananchi wa Tanzania na Uganda wakati wa utekelezaji wa mradi huo.
Mhe.
Ndejembi amesema mpaka sasa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la
Afrika Mashariki umefikia asilimia 79 na unatarajia kukamilika mwezi
Julai mwaka 2026, huku ukichochea ukuaji wa Uchumi na ongezeko la mapato
kwa nchi za Tanzania na Uganda, na kuongeza kuwa utakuwa na uwezo pia
wa kusafirisha mapipa 246,000 kwa siku pindi utakapokamilika.
Kwa
upande wake Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini kutoka Uganda Dkt.
Ruth Nankabirwa, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nia yake ya dhati kwenye utekelezaji wa
mradi huu ambao umekuwa na mafanikio makubwa na umeleta mapinduzi
makubwa kwa nchi za Afrika Mashariki.
Mhe.
Dkt. Ruth amesema kuwa, kuna haja ya watu wote wanaotekeleza miradi ya
kimkakati kama hii wanaopatiwa ajira kuwa na utaratibu maalumu wa
kuwatambua ili inapokuja miradi mingine wawe wanapewa nafasi kulingana
na uzoefu na uadilifu walionao katika utendaji wa kazi huku akitolea
mfano wa miradi ya gesi na umeme inayotarajiwa kutekelezwa na nchi hizi
mbili .
Mradi
wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani
mkoani Tanga una urefu wa kilomita 1,443 ambapo kilomita 296 ziko nchini
Uganda, na kilomita 1,147 ziko nchini Tanzania ambapo kwa upande wa
Tanzania kuna jumla ya vituo 4 vya kusukuma mafuta na Uganda kuna vituo 2
na kufanya jumla ya vituo vya kusukuma mafuta kuwa 6.
Post a Comment