Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Tuzo ambayo Tanzania imeshinda kuwa eneo bora la Utalii wa Safari Duniani (World’s Leading Safari Destination) kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar leo tarehe 05 Januari, 2026.
Akizungumza na
viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kabla ya kupokea tuzo hizo,
Rais Samia aliipongeza sekta ya utalii kwa kuendelea kuitangaza Tanzania
kimataifa na kuifanya kuwa miongoni mwa nchi vinara wa utalii barani
Afrika na duniani kwa jumla.
Tuzo hiyo iliyotolewa na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) yenye Makao Makuu yake Jijini London, Uingereza ambapo pia Miongoni mwa tuzo zilizopokelewa ni ya Tanzania kutangazwa kuwa Eneo Bora la Utalii wa Safari Duniani (World’s Leading Safari Destination)
Ikumbukwe kuwa hifadhi
ya Taifa ya Serengeti imetunukiwa tuzo ya Hifadhi Bora Duniani (World’s
Leading National Park), hatua inayozidi kuimarisha hadhi ya Tanzania
kama kitovu cha utalii wa asili na uhifadhi.
Baada ya kupokea
tuzo hizo, Rais Samia alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika
uhifadhi, huduma bora kwa watalii na utangazaji wa vivutio vya utalii.
Hata hivyo tuzo hizo zinaongeza chachu ya kutambua mchango wa Tanzania katika kukuza na kuendeleza utalii kwa viwango vya juu vya kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na
Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kabla ya kukabidhiwa Tuzo tatu
ambazo Tanzania imeshinda katika Utalii, Afrika na Duniani. Kikao hicho
kilifanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Januari, 2026.
| Muonekano wa Tuzo tatu za “WORLD TRAVEL AWARDS” ambazo Tanzania imeshinda. |
Post a Comment