Leo Senegal imeibuka mabingwa wa Africa Cup of Nations 2025 baada ya kuifunga Morocco 1–0 kufuatia msoto mkali wa muda wa ziada wa dakika 120 (extra time).
Goli la ushindi lilifungwa na Pape Gueye katika dakika za mwanzo wa muda wa ziada kwenye dakika ya 94 kufuatia mshituko wa mchezo.
Ikumbukwe kuwa Fainali ilikuwa ya msisimko mkubwa na ilijaa drama, ikianza kwa timu zote kushindana vikali na goli kutofungwa ndani ya dakika 90 za kawaida.
Kabla ya goli la Senegal, Morocco walipewa penalti mwishoni mwa muda wa kawaida lakini mpira uliokolewa na kipa wa Senegal, Edouard Mendy, huku mchezo ukielekea muda wa ziada.
Baada ya kuingia extra time, Pape Gueye alifunga goli la ushindi kwa Senegal, na kuifanya timu yake iwe bingwa wa Afrika.
Mechi ilikuwa na matukio ya ushindani mkali na aina mbalimbali ya maamuzi ya VAR, huku mashabiki wengi wakizungumzia uamuzi wa penalti na uchezaji wa mchezo.
Senegal imekuja na ushindi huu licha ya kutokuwa na baadhi ya wachezaji muhimu kutokana na adhabu au majeraha kabla ya mechi.
Senegal wameweza kushinda taji hili la Afrika mara nyingine tena, wakionyesha umoja, ustadi na kujitolea kubwa kwenye mchezo ulioitamba sana kwa mashabiki wa soka barani Afrika.
Aidha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Mhe. Paul Makonda, alikuwa nchini Morocco na amekuwa miongoni mwa viongozo wa Africa walioshuhudia mashindano ya AFCON 2025 na kuiwakilisha vyema Tanzania
Waziri Makonda alienda nchi humo akiwa na ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Tanzania kuhusu utayari wa Tanzania kushiriki kama mwenyeji wa AFCON 2027.




إرسال تعليق