BALOZI WA CANADA NCHINI AFANYA ZIARA BARRICK BULYANHULU NA KUPONGEZA UENDESHAJI WA MGODI KWA VIWANGO VIKUBWA SAMBAMBA NA KUFANIKISHA MIRADI YA KIJAMII


Balozi wa Canada nchini, Mheshimiwa Emily Burns, akiangalia mashine ya teknolojia ya kisasa ya uchimbaji madini bila kulazimika kushuka chini ya ardhi alipotembelea mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Balozi wa Canada nchini , Mheshimiwa Emily Burns akiangalia moja ya vifaa vilivyo chini ya mgodi alipotembelea sehemu ya chini ya mgodi (underground) kwenye mgodi wa Barrick Bulyanhulu , wa kwanza kushoto ni Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido.
Balozi wa Canada nchini , Mheshimiwa Emily Burns (wa pili kutoka kulia) akiangalia shughuli za uzalishaji chini ya mgodi (Underground) kwenye ziara yake ya kikazi katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu kulia ni Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bugarama , Dkt. Beatha Alistides akibadilishana mawazo na Balozi wa Canada nchini , Mheshimiwa Emily Burns, alipotembelea hospitali hiyo ambayo imefadhiliwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Balozi wa Canada nchini, Mheshimiwa Emily Burns akitembezwa katika maeneo ya kituo cha afya cha Bugarama
Balozi wa Canada nchini, Mheshimiwa Emily Burns, akifuatilia wasilisho kuhusiana na shughuli za Barrick nchini alipofanya ziara ya kikazi katika mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido akiwa kwenye kikao kwenye ujio wa Balozi wa Canada nchini Mheshimiwa Emily Burns (hayupo Pichani) alipotembelea mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick wakati wa mkutano na Balozi wa Canada nchini , Mheshimiwa Emily Burns alipotembelea mgodi wa Bulyanhulu.

                          **
Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Emily Burns, amefanya ziara ya kikazi katika mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga na kupongeza uendeshaji wa mgodi huo kwa viwango vya kimataifa sambamba na kufanikiwakutekeleza malengo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa vitendo.

Mhe. Burns, katika ziara hiyo ametembelea maeneo ya uzalishaji na kuona jinsi kampuni ya Barrick ilivyowekeza katika matumizi ya teknolojia za kisasa na zenye usalama kwa wafanyakazi katika shughuli za uchimbaji ambapo pia alitembelea baadhi ya miradi ya kijamii iliyotekelezwa kwa fedha za uwajibikaji kwa jamii kutoka mgodi wa Barrick Bulyanhulu ambayo ni kituo cha afya cha Bugarama na shule ya sekondari ya Bugarama.

Akiongea baada ya ziara hiyo Balozi Burns, ametoa pongezi kwa kampuni ya Barrick nchini kwa kuendesha migodi yake nchini kwa weledi mkubwa sambamba na kuhakikisha uwekezaji wake unaleta manufaa kwa jamii zinazozunguka maeneo ya migodi kupitia utekelezaji wa miradi ya kijamii na kutoa mchango wa ukuzaji uchumi wa taifa kwa ujumla kupitia kulipa kodi Serikali na kupanua wigo wa ajira kwa watanzania walioajiriwa migodini na wale wenye ajira zisizo za moja kwa moja ikiwemo wazabuni wanaofanya kazi na migodi.

"Nachukua nafasi hii kuipongeza kampuni ya Barrick kupitia Mgodi wake wa Barrick Bulyanhulu kwa jinsi unavyoendesha shughuli zake za uzalishaji kwa weledi kwa kuzingatia Usalama kwa Wafanyakazi wake na kwa jinsi unavyoshirikiana na Serikali na Jamii inayozunguka mgodi kwa kuwawezesha miradi ya maendeleo pamoja na vikundi mbalimbali vya wajasiriamali",amesema Balozi Emily Burns.

Naye Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido, ametoa shukrani kwa Balozi wa Canada nchini kwa kutembelea mgodi wa Barrick Bulyanhulu na kutembelea baadhi ya miradi ya kijamii iliyotekelezwa na mgodi huo ambayo imelenga kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi maeneo ya jirani na mgodi na jamii kwa ujumla.

"Kwetu ziara hii ni chachu ya kujifunza na kupokea maoni kutoka kwa wadau ili kuongeza jitihada za kufanya vizuri zaidi",amesema.

Dkt. Ngido ameongeza kuwa dhamira ya kampuni ya Barrick inayoendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals ni kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na mahitaji muhimu ili kunufaika na uwekezaji wake nchini.

Aidha ameongeza kuwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii ni mkakati endelevu wa kampuni ya Barrick unaojumuisha ushirikiano na wadau na vipaumbele ambavyo vimelenga kufanikisha kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zinazoishi kwenye maeneo yaliyopo Jirani na migodi yake sambamba na kufanikisha utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Dunia (SDGs).
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA