NSSF YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NA KUPOKEA TUZO KWA UZINGATIAJI WA SHERIA YA SERIKALI MTANDAO, VIWANGO NA MIONGOZO



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeibuka mshindi wa kwanza na kutunukiwa tuzo kwa Taasisi zilizofanya vizuri katika uzingatiaji wa Sheria ya Serikali Mtandao, viwango na miongozo kwa taasisi zilizo katika ngazi ya nne ya ukomavu wa TEHAMA Serikalini.

Tuzo hiyo ilitolewa na Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, na kupokelewa na Bw. Donald Mhaiki, Mkurugenzi wa TEHAMA wa NSSF.

Hafla ya utoaji wa tuzo hiyo ilifanyika wakati wa kilele cha Kikao cha 6 cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha International Conference Centre (AICC), jijini Arusha.

Ushindi huo unaonesha jitihada za NSSF katika kuimarisha matumizi ya TEHAMA na kuzingatia kikamilifu sheria, viwango na miongozo ya Serikali Mtandao nchini.







Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA