WANANCHI IDODI WAMLILIA LUKUVI


Wananchi wamlilia aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu na Mbunge wa Jimbo la Isimani Marehemu William Lukuvi kwa kazi nzuri alizozifanya wakati akitekeleza majukumu yake katika sekta mbalimbali serikalini na kuwaletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.


Hayo yamelezwa kwa wakati tofauti hii leo 30 Machi, 2026 wakati mwili wa marehemu Lukuvi ulipowasili Kijijini Kwake Kata ya Idodi, Wilaya ya Iringa Vijijini ambapo ndipo kunatarajiwa kuwa makazi yake ya milele mara baada ya ibada ya mazishi kijijini hapo.


Wananchi hao wameonesha simanzi kubwa na kumkumbuka kama kiongozi shupavu, na mtetezi wa wanyonge hususan kwa wakazi wa Jimbo Lake la Isimani mkoani Iringa.


Akizungumza na waandishi wa habari Mmoja wa waombolezaji Bw. Kombo  Jumbe amesema Marehemu William Lukuvi aliasisi utaratibu wa kliniki za ardhi wakati akiwa anahudumu kama Waziri wa Ardhi na hivyo kuwezesha wananchi kuhudumiwa kwa  urahisi na kwa haraka.


“Marehemu Lukuvi alituwezesha sisi hupata huduma kwa haraka hasa zilizohusu masuala ya migogoro ya ardhi na kufanya kufikiwa kwa urahisi na watoa huduma katika wizara ya ardhi  na yeye ndiye aliyezindua upatikanaji wa hati za ardhi na kufanya zoezi lile kuwa endelevu” alieleza


Kwa upande wake Bw. Frank Mbindile Mkazi wa Kijiji cha Magozi Wilaya ya Iringa amesema Marehemu William Lukuvi alikuwa ni mtu anayependa kusikiliza shida za watu kwa makundi na hata shida za mwananchi mmoja mmoja na kukiri kuwa wamepoteza mtu muhimu na Lulu kwa Taifa. 


“Ni aina ya kiongozi anayeamini katika kusimamia mambo ya msingi kwa ajili ya maslahi mapana ya wananchi na akizungumza jambo alikuwa anauwezo wa kulisimamia, hivyo wanaisimani tumepoteza kiongozi mkubwa,” alieleza.











Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA