Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Alban Mark Kihulla amewatembelea na kuzungumza na watumishi wa Wakala huo Mkoa wa Arusha tarehe 31 Julai 2026.
Lengo kuu la ziara hiyo lilikuwa kusikiliza changamoto za watumishi, kuwapongeza kwa utendaji wao, na kuwapa mwelekeo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wakala.
Akizungumza na watumishi hao, Afisa Mtendaji Mkuu aliipongeza Ofisi ya Mkoa kwa kazi nzuri ya uhakiki wa vipimo wanayoendelea kufanya.
Alisema mafanikio ya WMA yanategemea uadilifu, umahiri na nidhamu ya kila mtumishi.
Aidha, aliwataka watumishi kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi na kuzingatia maadili ya kazi. “Tuwe mabalozi wazuri wa WMA. Kila mteja tunayemhudumia ni fursa ya kujenga taswira nzuri ya Wakala,” alisisitiza.
Kwa upande wao, watumishi wa Mkoa wa Arusha walimshukuru Mtendaji Mkuu kwa uongozi wake wenye 'kuonesha njia' na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii.
Katika ziara hiyo ya Afisa Mtendaji Mkuu, watumishi walipata nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo mbalimbali ya kuboresha utoaji huduma ya vipimo katika Mkoa huo.




Post a Comment