NJAMA AIBUA VIASHIRIA VYA RUSHWA MIGOGORO YA ARDHI KOROGWE


Mbunge wa Korogwe Mjini, CPA Charles Mhando Njama, amesema migogoro mingi ya ardhi katika Kata ya Old Korogwe ina viashiria vya rushwa, akitaka hatua zichukuliwe kubaini chanzo cha migogoro hiyo.


Njama amesema hali hiyo inaonekana kuanzia katika Serikali za Mitaa hadi ngazi ya Kata na katika baadhi ya mamlaka zinazohusika na masuala ya ardhi, akieleza kuwa changamoto hizo zimekuwa zikichangia migogoro ya ardhi kuwa mikubwa.


“Haiwezekani huyu mtu anacho kiwanja, anazo document zote, halafu ameleta malalamiko yake kwenye vyombo vya kuweza kutoa utatuzi, bado anaonekana hana haki. Hapana, nadhani kuna tatizo kubwa,” amesema Njama.


Amesema kuna umuhimu wa kuchunguza kwa kina namna migogoro ya ardhi inavyoshughulikiwa katika eneo hilo, hasa pale ambapo wananchi wanawasilisha nyaraka zinazodaiwa kuthibitisha umiliki wa maeneo yao lakini bado wanakosa suluhisho la kero zao.


Njama ameyasema hayo Septemba 23, 2026, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi wa Mtaa wa Lwengela Darajani, Kata ya Old Korogwe, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.


Amesema kutatuliwa kwa migogoro hiyo kunahitaji mamlaka zinazohusika kusimamia haki na kuhakikisha malalamiko ya wananchi yanashughulikiwa kwa kuzingatia nyaraka na taratibu za kisheria.



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA