Na, Mwandishi wetu - Rukwa
Watu watatu wameuawa, wawili kujeruhiwa na wengine 25 kukamatwa kufuatia vurugu zilizotokana na mgogoro wa wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco G. Chilya, amesema kati ya waliokamatwa, wanane wanahusishwa na mauaji na 17 na vurugu, huku 10 wakiwa wafugaji na 15 wakulima.
Amesema vurugu hizo zimesababisha uharibifu wa mali, ikiwemo kuchomwa kwa ofisi za Serikali na kuharibiwa kwa gari la Polisi, huku operesheni ikiendelea kuwabaini wahusika wengine.
Kwa mujibu wa Polisi, tukio lilianza Septemba 17, 2026, baada ya mfugaji Shimbi Upole Shimbi, 45, kudaiwa kuporwa ng’ombe 180 na kundi la watu waliodaiwa kuwa wakulima.
Septemba 18, mchungaji Msanja Shimbi Upole alikutwa ameuawa na mwili wake kuzamishwa kwenye matope katika Mto Chermambo, Kijiji cha Chinunje.
Baada ya tukio hilo, wafugaji walivamia Vijiji vya Chikomo na Chinunje, ambako Mohamed Kasim Chabwela, 58, aliuawa, huku Yusuph Yasin Bakili, 42, na Rashid Ally Ahmad, 49, wakijeruhiwa.
Post a Comment