Airtel Tanzania imeibuka mshindi wa pili kwenye kutoa gawio kwa mwaka wa fedha 2024/25, imewasilisha hundi ya Sh bilioni 73.9 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ametoa shukrani kwa uongozi wa kampuni hiyo – hundi hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi Eliudi Sanga (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu Charles Kamoto – katika hafla ya Siku ya Gawio iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Airtel Tanzania, kama mtoa gawio namba mbili nchini kwa mwaka wa fedha 2024/25, imewasilisha hundi ya Sh bilioni 73.9 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya Siku ya Gawio iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel, Eliudi Sanga (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji, Charles Kamoto, wameongoza makabidhiano hayo rasmi.
Airtel Tanzania imetunukiwa tuzo kama mtoa gawio namba mbili nchini kwa mwaka wa fedha 2024/25 baada ya kutoa Sh bilioni 73.9, katika hafla ya Siku ya Gawio iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi, Eliudi Sanga (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji, Charles Kamoto, wamepokea tuzo hiyo kutoka kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan (kulia).
Airtel Tanzania imetunukiwa tuzo kama mtoa gawio namba mbili nchini kwa mwaka wa fedha 2024/25 baada ya kutoa Sh bilioni 73.9, katika hafla ya Siku ya Gawio iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi, Eliudi Sanga (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji, Charles Kamoto, wamepokea tuzo hiyo kutoka kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan (kulia).
***
Dar es Salaam, Juni 10, 2025 - Airtel Tanzania imeibuka nafasi ya pili katika mashirika yaliyotoa gawio kubwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2024/25, na kuwasilisha hundi ya Shilingi bilioni 73.9 kwenye hafla ya siku ya Gawio iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo iliandaliwa Ofisi ya Msajili wa Hazin na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Utoaji wa Gawio na Mchango huo sio tu inadhihirisha ufanisi na kukuaji kwa Airtel kibiashra bali unaonyesha jinsi Airtel ilivyojidhatiti kuendelea kuwa mdau muhimu wa maendeleo ya taifa kupitia ushirikiano wa kimkakati baina ya sekta ya umma na sekta binafsi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shukrani kwa mashirika ya sekta binafsi kwa kuchangia kiasi cha trilioni 1.28 kwa mwaka huu. Pia alisisitiza kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ili kuendelea kuchochea uwekezaji na kuongeza kasi ya ukuaji kiuchumi.
Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa siku ya hiyo inadhihirisha muelekeo wa serikali katika uendeshaji wa mashirika ya umma huku akiyataka yaweze kuzalisha na kujiendesha yenyewe.
“Nawapongeza wote ambao mmeweza kuchangia. Siku hii inatoa fursa kwa wananchi kuona namna mashirika mbalimbali yanawajibika kwao. Niyatake mashirika na taasisi kuongeza ubunifu kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji na kutatua changamoto zinazowakabili,” amesema Dkt. Samia.
Pia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ametoa rai kwa mashirika ambayo yanamilikiwa na serikali kwa hisa yahakikishe yanatumia kikamilifu mifumo ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi na tija na uwazi katika utendaji.
Tangu mwaka 2019, Airtel Tanzania Plc pamoja na Airtel Money Tanzania Ltd zimechangia jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 280 kwa serikali. Kupitia umiliki wa serikali kwa asilimia 49, kampuni hii imebaki kuwa mfano wa namna ushirikiano na sekta binafsi unaweza kuleta manufaa ya muda mrefu.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Eliudi Sanga, amebainisha kuwa kujituma kwa Airtel kuna mchango mkubwa katika kuchochea mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.
“Airtel Tanzania inajivunia kuwa mshirika wa kuaminika katika safari ya maendeleo ya taifa. Uwekezaji wetu unaendana na vipaumbele vya kitaifa vya Serikali kwa kupanua miundombinu ya kidijitali kwa kuchangia upatikanaji uliojumuishi na wezeshi wa uchumi wa kidijitali,” amesema Sanga.
Kwa upande wake, Charles Kamoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, alisisitiza juu ya malengo ya kampuni kuwezesha ukuaji jumuishi na uwezeshwaji wa kidijitali.
“Mchango wa gawio letu ni kielelezo cha msimamo wetu katika kuchagiza kwenye maendeleo endelevu ya Tanzania. Hii inaakisi namna sera ya serikali inavyoendana na ubunifu wa sekta binafsi katika kuleta maendeleo jumuishi na kuelekea katika uchumi wa kidigitali,” amesema Kamoto.
Kamoto amesema Airtel inajivunia kuiunga mkono serikali kupitia uwekezaji wake kupitia upanuzi wa mtandao, unafuu wa vifaa vya mawasiliano na majukwaa ya kidijitali nchini Tanzania.
Airtel Tanzania, kama mtoa gawio namba mbili nchini kwa mwaka wa fedha 2024/25, iliwasilisha hundi ya Sh bilioni 73.9 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya Siku ya Gawio iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel, Eliudi Sanga (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji, Charles Kamoto, wameongoza makabidhiano hayo rasmi.

Post a Comment